NAY WA MITEGO AWASILI CENTRAL POLISI KUITIKIA WITO JUU YA WIMBO WAKE WA "AMKENI"


 Msanii Nay wa Mitego leo ameitikia wito na amewasili katika kituo cha Polisi Central Jijini Dar es salaam kuhusu wimbo wake wa ‘Amkeni’ ambao hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuufungia kuchezwa katika vituo vyote vya Radio na Televisheni.


Nay aliwasili akiwa ameambatana na Mwanasheria wake Jebra Kambole kabla ya kuingia dani Nay alizungumza na waandishi akisema “Ukiwa sauti ya Watu kuja sehemu kama hii ni kawaida, mimi ni sauti ya Watu acha nikawasikilize nitakuwa na cha kuongea lakini kwa sasa sina, nimeambiwa tu ni wimbo wangu wa ‘amkeni’ kwahiyo nataka nikajue umefanya nini, kuna tatizo gani”


No comments

anonymous