Select Menu

Slider

Travel

Performance

Cute

My Place

Photos

Racing

Videos


Jerry MuroMsemaji wa Timu ya Yanga
Na Ripota wa Globu ya Jamii

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeishukia bodi ya Ligi kwa kile walichodai kuwa wamechakachua kanuni kwa kuiruhusu Timu ya Simba kumtumia mchezaji Ibrahimu Hajibu na kuitaka sheria zichukue mkondo wake huku wakigomea mechi yao dhidi ya JKT Ruvu kusogezwa mbele.

Akizungumza kwenye Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Msemaji wa Yanga Jerry Muro amesema Bodi ya Ligi inayumbisha soka la Tanzania kwa kupindisha sheria na kitendo walichofanya ni cha ubabaishaji na hawawezi kukikalia kimya.

"Umeshaona wapi mtu anakosa, anakaa kujadili adhabu ya kupewa na mtoa adhabu, Tanzania ni ya kwanza, halafu eti tunataka soka letu lisonge mbele, litasonga mbele kwa stahili hii?"alisema kwa kuhoji.

Katika barua ya Februari 27 iliyosainiwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Fatuma Abdallah kwenda kwa katibu mkuu wa Simba Steven Ally ilisema "rejea barua yako ya Februari 25 yenye kumbukumbu namba SSC/29/2015/07/GS  kwa niaba ya bodi ya ligi tumezingatia maombi ya timu yako kutaka kwa mchezaji Ibrahimu Hajibu aruhusiwe kucheza mchezo wa Simba dhidi ya Prisons na Simba dhidi ya Yanga na asicheze mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Kwa kuzingatia mabadiliko ya katiba yaliyofanyika hivi karibuni, kwa barua hii mchezaji yuko huru kucheza katika mchezo wa Simba na Yanga." ilisema sehemu ya barua hiyo na nakala kutumwa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Kamati ya waamuzi, msimamizi wa kituo Dar es Salaam na Yanga.

Hata hivyo Yanga walidai kuwa hawawezi kukubaliana na jambo hilo kwa kuwa mabadiliko hayo ya katiba yalipendekezwa na bado hayajapata baraka ya mkutano mkuu.

Kwa mujibu wa kanuni ya 37 (4) ya Ligi kinachozungumzia udhibiti kwa wachezaji inasema 
klabu zinatakiwa zitunze kumbukumbu za wachezaji wake waliyoonyeshwa kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na  magoli 3, halikadhalika mchezaji anatakiwa atunze kumbukumbu zake za kadi na iwapo atacheza akiwa anatakiwa kutocheza kwa ajili ya kadi tatu za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo.

Wakati huo huo Yanga wamegomea mechi yao na JKT kusogezwa mbele na kudai kuwa Machi 11 hawatapeleka timu uwanjani kwa kuwa watakuwa wakijiandaa na mchezo wao na Plantiam ya Zimbabwe.

Katibu mkuu wa Simba Steven Ally alipoulizwa kuhusiana na suala la kuandika barua hiyo alisema "Ni kweli niliandika kama kupinga kanuni walitakiwa kupinga kwenye kikao cha bodi ya Ligi sio sasa, kanuni ilishapitishwa, na Yanga wanayo nakala tunashangaa sasa hivi wanavyopinga maamuzi ya TFF na bodi  ya Ligi basi waende Fifa."

Naye Katibu mkuu wa Simba Steven Ally alipoulizwa kuhusiana na suala la kuandika barua hiyo alisema "Ni kweli niliandika kama kupinga kanuni walitakiwa kupinga kwenye kikao cha bodi ya Ligi sio sasa, kanuni ilishapitishwa, na Yanga wanayo nakala tunashangaa sasa hivi wanavyopinga maamuzi ya TFF na bodi  ya Ligi basi waende Fifa."

"Tumejiandaa mechi yetu na JKT tunacheza kesho (leo), na Jumapili tunacheza na Simba, sasa bodi ya Ligi wanatuhujumu wanatupangiaje mechi tarehe 11 alafu tarehe 14 tucheze na Zimbabwe wanatutaka nini hao?" alihoji na kuongeza.

"Mkakati wetu ilikuwa tukimaliza mechi ya Jumapili akili yetu tunaelekeza kwa Zimbabwe, nasema tena Machi 11 hatupeleki timu tupo tayari kushuka daraja wakitaka waipeleke mbele zaidi tumalize na Zimbabwe."alisisitiza
-

Bonyeza hapa>>DOWNLOAD


- -

- -


 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiweka jiwe na msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40. Kulia kwake ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.6. Katikati ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili Kikweni kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.
 . Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma cha Msanja group kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Usangi kuhusu ujenzi wa barabara ya Kikweni-Usangi-Lomwe ambayo itaanza kujengwa hivi karibuni.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mama Ana Kilango Malecela katika sehemu ya Kihurio.Dkt. Magufuli ametangaza kujengwa kilomita tatu za lami katika eneo hilo pamoja na kuifanyia maandalizi ya kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Mkomazi-Same yenye urefu wa km 96.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kihurio Same Mkoani Kilimanjaro.
 Wakazi wa Usangi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
 Waziri wa Ujenzi akiwahutubia wakazi wa Gonja wakati akipita kukagua barabara ya Kihurio hadi Gonja maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
 
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Usangi mara baada ya kuwahutubia.
Picha ya Pamoja Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli katikati akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya na Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Wilaya za Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi
-

DSC_0113
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
WADAU mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi kuwa na tija kwa wananchi wake.
Yusuph alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitatu.
Alisisitiza kwamba kwa kuwa mradi huo utakuwa na mawasiliano ya kisasa, masomo kwa njia ya Tehama, tiba kwa kutumia mtandao wadau wamekusanyika mjini Bagamoyo kuangalia namna bora ya kuufanya mradi huo uwe endelevu hata kama UNESCO na mbia wake Samsung watajiondoa huko mbeleni.
Aliwataja baadhi ya wadau kuwa ni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Samsung, Unesco, wanakijiji wa Ololosokwan, waganga wa jadi wakunga, Taasisi ya elimu na Chuo cha Ufundi cha DIT.
Alisema changamoto ambazo zinaonekana ni lazima ziangaliwe ni pamoja na matumizi ya lugha hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa wengi wa wananchi wa Kimasai hawazungumzi Kiswahili fasaha.
“tunategemea sana Tehama kufanikisha mradi huu, na lugha inayoweza kutumiwa ni Kiswahili, sasa hili ni changamoto ni lazima kuangalia mawasiliano” alisema Yusuph na kuongeza kuwa kuwapo kwa radio ya jamii kutachangia kwa kiasi kikubwa kutoa nafasi ya wananchi wengi kujifunza Kiswahili.
Aidha alisema kwamba mambo mengine ambayo yanaangaliwa katika warsha hiyo ni matumizi ya Tehama (intaneti) na kutoa mafunzo ya namna ya kuhudumia na kufanyia matengenezo mitambo mbalimbali iliyomo katika mradi huo.
DSC_0141
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akishiriki kutoa maoni wakati wa warsha hiyo inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. Aliyesimama ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Alisema nia kubwa ya kukusanya wadau mbalimbali ni kuangalia utekelezaji wa nia ya mradi ya kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa jamii ya kimasaii ambayo kwa sasa utamaduni na uchumi wake unatishiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
“Tunataka maendeleo haya yasaidiwe na mawasiliano. Tunaangalia jinsi ya kutumia mawasiliano kuleta maendeleo” alisema Yusuph.
Alisema ni matumaini yao kwamba wabia wengine wa mradi huu ambao ni kampuni ya simu ya Airtel watatumia uwezo wao kuhakikisha kwamba kijiji hicho kinakuwa hewani muda wote kwa lengo la kurahisisha huduma zinazopatikana kwa njia ya mtandao hasa tiba.
Aidha alisema kwamba pamoja na kuleta maendeleo mradi huo unakusudiwa kuhamasisha amani kati ya koo na makabila mbalimbali yaliyopo wilayani Ngorongoro.
DSC_0082
Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi (wa kwanza kulia) akichangia maoni kwenye kikundi cha sekta ya Afya wakati wa kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili jamii ya wafugaji wa kijiji cha Ololosokwan katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali huku Mwenyekiti wa kikundi hicho kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman(katikati kulia) akiorodhesha maboresho ya changamoto hizo.
Katika warsha hiyo ambapo wadau wamegawanyika makundi mbalimbali ili kutengeneza hoja za kufanyia kazi kwa ajili ya kufanikisha masuala ya elimu na afya.
Katika elimu wameangalia vikwazo ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na watoto kuacha shule kwenda kuchunga mifugo.
Ili kukabiliana na kiwango kikubwa cha kutojua kusoma na kuandika kipaumbele kinachofikiriwa ni kuwafikia vijana hao wakiwa machungani kwa kuwapelekea mafunzo kwa njia ya mtandao.
Afisa Mipango wa Elimu wa Unesco, Jennifer Kotta alisema changamoto ya elimu katika kijiji hicho na majirani ni kubwa na kwamba wanachofikiria ni kutumia Tehama ambapo sasa watawafikia vijana kule waliko.
DSC_0110
Wadau mbalimbali wa Elimu, Afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi wanaoshiriki warsha ya wiki moja inayofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha dijiti cha Samsung cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Aidha wamepanga kufunza lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kutanua wigo wa majadiliano wa wakazi wa eneo hilo na watalii wanaofika na kupenda kununua kazi zao.
Warsha hiyo iliyofunguliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini inafanyika wakati vifaa vya kutengeneza kijiji hicho vikiwa vimeshaondoka katika bandari ya Dar es salaam.
Katika masuala ya Afya wadau wameangalia vipaumbele vinavyostahili sasa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mimba na mtoto.
Wamesema wanawake wa kimasai wanafanya shughuli nyingi kuanzia ujenzi wa makazi na ukamuaji wa maziwa hadi ulezi wa watoto na kusema katika mazingira hayo wanahitaji sana elimu ya uzazi salama.
DSC_0088
Mwenyekiti wa kikundi cha Sanaa na ubunifu kutoka UNESCO, Courtney Ivins (wa pili kushoto) wakijadiliana na wanakikundu wenzake kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utamaduni hususani kwa wakimama wa kimasai wanaotengeneza bidhaa za shanga jinsi ya kuziboresha na kuvutia watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro mpaka kijiji cha Ololosokwan pamoja na jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi iliyopo kwenye jamii za wafugaji.
DSC_0084
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye majadiliano na kikundi chake huku wakiangalia changamoto mbalimbali za masuala ya Tehama zinazoikabili kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuziboresha ikiwa ni maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0092
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki (wa kwanza kushoto) na wadau kutoka Ololosokwan wakianisha changamoto na utatuzi wa changamoto kwenye sekta ya elimu katika kuboresha utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigiti cha Samsung cha Ololosokwan wakati wa warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0097
-