Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Haitham Kim amefariki Dunia


TANZIA: Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva @haithamkim amefariki Dunia mchana huu katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.  kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya upumuaji.

Taarifa ya Msiba imethibitishwa na Dada wa Mume wa Hatham ambaye amezungumza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Haitham ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa #playboy na nyingine nyingi alizoachia hivi karibuni ameacha mume na mtoto mmoja

Vimba Media tunatoa salamu za pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Mashabiki wote wa muziki wa Haitham Kim. Hakika Sote kwake tutarejea. 🙏🏽

No comments

anonymous