Otile Brown Aonyesha picha za jumba jipya analojenga


Mwimbaji nyota kutoka  Kenya Otile Brown ameshare picha za jumba jipya analojenga na mashabiki wake wakifurahi.

Kupitia  kwenye Insta-stori zake Otile aliweka picha za jumba hilo na kuandika  kuwa yuko kwenye hatua za mwisho za ujenzi  kukamilisha jumba hilo ndani ya miezi 5 ijayo.

 Kwa kweli kununua nyumba si sawa na kujenga ... jengo ni maalum kujaribu kumaliza hii katika miezi mitano inshallah.  Ni miezi miwili sasa.

Otile ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaomiliki majumba maridadi nchini Kenya.  Katika siku za hivi karibuni, idadi kubwa ya watu mashuhuri wamekuwa wakiwekeza katika maeneo yao ya vijijini, kwa lengo la kumiliki eneo linalostahili kuitwa nyumbani. Mastaa wengine walioshiriki picha za nyumba zao ni pamoja na;  Jalang’o, Khaligraph Jones, Bahati, Mtayarishaji wa Muziki Teddy B, Mcheshi Oga Obinna, Anthony Ndiema na mwimbaji Sudi Boy na Timmy Tdat.

 Otile ameweka  picha za nyumba yake ikiwa ni  siku chache baada ya kutia saini mkataba wake mnono wa kwanza wa ubalozi. No comments

anonymous