Mwanga Hakika Microfinance Bank, benki mpya baada ya kuungana kwa benki tatu

 


Mwanga Community Bank Ltd, Hakika Microfinance bank Ltd na EFC Tanzania Microfinance zimefanikiwa kuungana na kuwa Bank moja ijulikanayo kama ‘Mwanga Hakika Microfiance Bank Ltd. hatua inayoashiria ukuaji wa sekta ya kibenki nchini.

Muunganiko huoumefanikiwakufuatiauthibitishokutokabenkiya Tanzania (BoT) pamojanaTumeyaushindani (FCC) nakupelekeakuundwakwaBenkimojayenyethamaniya 40.5 bilioniya mali.Pia, benkihiyoinatarajiakuongezanguvuyaushindanikatikasokonchini. 

 Muungano huo ulizinduliwa rasmi katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse na kushuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha.

 Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Eng. Ridhuan Mringoa lisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja na zenyekuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.

 “Tunaamini kwamba huu ni muda wa Kuimarisha sekta ya kibenki na hiiimejidhihirisha kwa baadhi ya benki ambazo ziliamua kuungana na kuunda benki moja imara. Sisi tumeamuakuungana ili kutengeneza benki kubwa na imara ambayo itasaidia kuongeza kasi yaukuaji wabiashara yetu,” alisema Eng. Mringo.

 Aliongeza kuwa kupitia benki hiyo wateja wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi na bidhaa zenye ubunifu katika mikopo na uhifadhi (savings) ambazo zitakuwa nafuu na za haraka.  “Kuanzia sasa mahitaji ya kila siku ya kibenki ya wateja wetu yataweza kutimizwa na benki hii mpya.

Tuna tegemea kukua kwa makusanyo ya akaunti za wateja kwa sababu benki hii itakuwa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedhaa pia Kupitia muungano huo, benki mpya itaweza kuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji huduma ikiwa na matawi saba (7) ambayo yataweza kuhudumia wateja 105,000 nchinzima"alisema Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard kibesse.

Alipongeza hatua iliyo chukuliwa na benki hizo na kwamba itasaidia katika uimarishaji wa sekta ya kibenki kwa kuhakikisha watu ambao hawajafikiwa na huduma wanapata nafasi hiyo. 

Pia, alisema itasaidia katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwani benki hiyo itakuwa na wigo mpana wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali wadogo na wakati jambo litakalo changia kuleta ujumuishwaji wa uchumi.

 “Sekta ya kibenki ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia ajira na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo na zakati kupitia mikopo nafuu.Tunaamini kuwa benki hii itachangia kati uimarishaji wa sekta hii na hatimaye kuongeza ujumuishwaji wa watu kiuchumi hapa nchini,” alisema Dk. Kibesse.

 Takwimu: 

 Awali, Benkiya Mwanga ilikuwa na mali zenye thamaniya Sh21.6 bilioni huku Hakika benki ikiwa na 6.669 na EFC ikiwana 12.253 bilioni na kufanya jumla ya benki hiyo kuwa na mali zenye thamani ya 40.5 billion.

 Kwa upande wa amana za wateja, Mwanga ilikuwa na 14.8 bilioni, Hakika 2.7 bilioni na EFC 5.96 bilioni. Jumla ya mikopo ambayo imetolewa na benki hizo mpaka sasa ni 27.1 bilioni.


No comments

anonymous