Vanessa Mdee azindua programu ‘app’ ya simu ya VEE MONEY kwa ajili ya mashabiki wake.Vanessa Mdee mwanadada anayetikisa soko la mziki nchini Tanzania ameendelea kuwa na wiki ya kihistoria ambayo ilianza kwa kuzindua albamu yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake na wadau wengine wa mziki nchini siku ya Jumatatu.

Leo Vanessa amezindua programu ‘app’ yake mpya ya simu ya VEE MONEY ambayo inapatikana bure kupitia ‘Google Play store’ na ‘Apple store’. Programu hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani, Converge Media, ni sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata maudhui ya kipekee ya Vanessa kama vile; nyimbo, video, picha, na kuona kurasa zake za kijamii.

‘Kwanza natoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea albamu yangu kwa mikono miwili, na sasa natumaini app hii itazidi kutuweka karibu’ alisema Vannesa.
Vanessa atakamilisha wiki yake ya kihistoria kesho kwa kuweka sahihi katika album zake tukio ambalo litafanyika eneo la Mlimani City Mall kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

No comments

anonymous