Mama Samia Suluhu azindua rasmi kampeni ya Uzalendo na Utaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Samia Suluhu Hassan amezindua kampeni ya Uzalendo na Utaifa 'Nchi Yangu Kwanza' itakayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa.

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpoto Thearte Gallary ina nia kukumbushana suala la uzalendo ikiwemo kuepusha rushwa, maadili ya viongozi wa Umma pamoja  na kukufua uwajiikaji kwa watumishi wa umma.

Makamu wa Rais amemuomba Waziri Dkt.Mwakyembe aunde kamati ndogo itakayozunguka katika maeneo yote ya nchi kuhamasisha uzalendo.

" Uzalendo siyo kipaji bali  unajengwa  na kuaandaliwa na jamii husika, kampeni hii inatoa fursa ya kuelimisha vijana umuhimu wa tamaduni,sanaa,mila na maadili ya kitanzania. Tufanye mambo kwa wakati , wakati tunawakati ,tuutumie wakati vizuri kutekeleza mambo yetu," alisema makamu wa Rais " Makamu wa Rais .

Kwa upande wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kupenda mila na tamaduni za ndani kwa kuwa hizo ndio alama ambazo zinaitambulisha nchi na kuzitofautisha na mataifa mengine. 

"Tuwe wazalendo kwa kupenda sanaa na tamaduni zetu zinazotutambulisha sisi kama taifa, ufanye kazi kwa bidii ili tuzalishe mali kwa wingi na kujenga taifa letu huo ndio uzalendo," Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa

"Tunayosababu ya Kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwahamasisha watanzania kuwa wazalendo. Suala la uzalendo kwa nchi yetu siyo jambo geni hivyo ni wajibu wetu kuudumisha kwa maslahi ya taifa letu na ili kufikia uchumi wa viwanda ni wajibu wetu kuwa wazalendo kwa kusimamia rasilimali zetu," aliongeza Majaliwa.

Naye Waziri wa Habari Dkt Mwakyembe alisema uzalendo ni kuthamini vitu vyetu pamoja na lugha ya kiswahili amayo imekuwa kivitio duniani kote.

"Kufikia 2063 kiswahili itakuwa lugha kuu barani Afrika na utambulisho wa mtu mweusi, huo ndio uzalendo na maendeleo ya Sayansi na teknolojia katika Tehama imesababisha misingi bora ya utamaduni wetu kupata nyufa"Dkt.Mwakyembe.

Waziri amewataka watanzania kuipokea kampeni hiyo kwa mikono miwili kwa kuwa ni kampeni ambayo inaenda kulifanya taifa la watu ambayo wapo tayari kufa kwaajili ya nchi yao.

Katika usiku huo wasanii wakiongozwa na Mrisho Mpoto waliimba wimbo maalum kwaajili ya kampeni hiyo. Wasanii hao ni pamoja na Fid Q, Ray C, Witnes, Kassim Mganga pamoja na wengine.

No comments

anonymous