RaisMagufuli afanya ziara ya kushtukiza Tazara na Ubungo, Aamuru Jengo la TANESCO livunjwe


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili jijni Dar es salaam muda huu akitokea kijjini kwake Chato, mkoa wa Geita, na kupokelewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine na mara baada ya kuwasili ametembelea na kukagua ujenzi wa flyover Tazara pamoja na  ujenzi wa daraja la ghorofa tatu barabara ya ubungo, aamuru sehemu ya jengo la TANESCO na jengo la Idara ya maji zilizo kwenye eneo la barabara zivunjwe


 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakitembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Flyover ya TAZARA mapema leo,kulia ni Mkuu wa mkoa Dar Mh Paul Makonda.Wakati huo huo  pia Rais Dkt Magufuli ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’, katika ukaguzi wa Ubungo Rais Dkt Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha ujenzi wa mradi huo.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mapema leo mbele ya baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) walikuwepo katika eneno hilo, mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Flyover ya Tazara,kushoto ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda walipokuwa wakiwasili maeneo ya Ubungo na kuanza kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’, ambapo katika ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha ujenzi wa mradi huo.
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza mmoja wa Wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi wa barabara za juu ‘Ubungo Interchange’,mapema leo 
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi mbalimbali waliokuwa wamejitokeza mapema leo,wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli (pichani kulia),alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu za Ubungo ‘Ubungo Interchange’,mapema leo jijini Dar.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa mradi huo wakishangilia wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao 
 Maendeleo ya Ujenzi wa Flyover ya Tazara jijini Dar Es Salaam kama unavyoonekana pichani mapema leo mchama,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassani walitembelea na kujionea maendeleo yake,ambapo Mkandarasi wa mradi huo amesema kuwa asilimia 63 ya ujenzi umekamilia na kwamba Flyover hiyo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 8,2018 badala ya Desemba 2018.
No comments

anonymous