Ndikumana Mume wa Irene Uwoya wa Zamani Afariki Dunia

Habari ya kusikitisha, mume wa zamani wa Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia. Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda. Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya. 

Mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia. Mpaka Sasa Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini . Mwili wake umehifadhiwa katika monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala. #harakatizabongo

No comments

anonymous