Alichokisema Lulu kuhusu Kesi yake


Ikiwa imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.

Lulu ameyasema hayo leo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa. “Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.

Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.

Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.

Elizabeth Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo April 7, 2012 .



Film, also called a movie, motion picture, theatrical film, or photoplay, is a series of still images that when shown on a screen create an illusion of motion images (due to the phi phenomenon).

This optical illusion causes the audience to perceive continuous motion between separate objects viewed rapidly in succession. The process of filmmaking is both an art and an industry.

 A film is created by photographing actual scenes with a motion picture camera; by photographing drawings or miniature models using traditional animation techniques; by means of CGI and computer animation; or by a combination of some or all of these techniques and other visual effects.

No comments

anonymous