TID kuchukizwa na kitendo cha Ben Pol Kuimba wimbo wake na kumtusi ni sawa..?

Ben Pol amekuwa mbunifu sana katika show zake na wakati mwingine hutumia nyimbo tofauti za wasanii wenzake katika stage, katika tamasha la Fiesta liloisha Ben Pol aliwahi kuimba wimbo wa TID "Nyota Yangu" wakati mwingine msanii hutumia kazi ya msanii mwenzake ni kama vile kuonyesha anakubali na anapenda kazi za msanii huyo lakini kwa TID imekuwa tofauti na kuonekana kuchukizwa na kitendo cha Ben Pol kuimba wimbo wake.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo, East Africa Radio kuwa atazungumza na wakubwa wake pamoja na wanasheria wake ili kumchukulia hatua Ben Pol.

“Nina kesi moja na Ben Pol, huyo jamaa kwenye concert moja kubwa sana halafu ilikuwa na sponsored na wamemlipa hela nyingi lakini kwenye nyimbo zake alizofanya katika playlist yake kaweka wimbo wangu anaimba although those sponsor don’t like me kabisa because am not performing, am not there” amesema TID.

“Wao wanaimba unawalipa what about me, what about my copy right, ni makosa na nitaongea na wakubwa ila alichokifanya ni kuonyesha how is weak” ameongeza.

Alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha anachohitaji kutokana na hilo, alijibu; baada ya kuongea na wanasheria wangu ndio nitajua, kwani yeye analipwa kiasi gani hadi anaimba wimbo wangu”.

Katika tamasha la Fiesta lilofanyika November 25, 2017 Dar es Salaam, Ben Pol baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa Moyo Mashine aliunganisha na wimbo wa TID ‘Nyota Yangu’.

Je unamaoni gani kuhusu hii.... weka comment yako hapo chini.


Sauti ya TID akiongea


________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Bongo flava is the nickname for Tanzanian hip hop music. The genre developed in the 1990s, mainly as a derivative of American hip hop, with additional influences from reggae, R&B, afrobeat, dancehall, and traditional Tanzanian styles such as taarab and dansi, a combination that forms a unique style of music. Lyrics are usually in Swahili or English.

The name "bongo flava" is a corruption of "bongo flavour", where "bongo" is the plural form of the Swahili word ubongo, meaning "brain", and is a common nickname used to refer to Dar es Salaam, the city where the genre originated. In the bongo flava, the metaphor of "brains" may additionally refer to the cunning and street smarts of the mselah

No comments

anonymous