Makamu wa rais Mama Samia amjulia hali Tundu Lissu, atuma salamu kwa Rais


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.
“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali leo tarehe 28 Novemba, 2017 jijini Nairobi nchini Kenya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali leo tarehe 28 Novemba, 2017 jijini Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Alicia Magabe na kulia ni msaidizi wa Makamu wa Rais Bw. Waziri
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana (kulia) walipofika hospitalini hapo kumjulia hali. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Bi. Alicia Magabe na wa pili kulia ni msaidizi wa Makamu wa Rais Bw. Waziri
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Bi. Alicia Magab

No comments

anonymous