Ben Pol kushiriki filamu Paris


Msanii Ben Pol akiwa na wenyeji wake mara baada ya kuwasili Paris Ufarnsa, Msanii huyo anashiriki tamasha maalum nchini humo litakalofangika Nove 18, mwaka huu, kulia kwake ni David Shenyagwa na kushoto ni Chami Mtungwa 


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol' ameenda nchinj Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum ya MAÜA Association pamoja na uzinduzi wa Filamu ya NDOTO utakaofanyika Tarehe 18 Novemba 2017 mjini Paris nchini humo.

Ben Pol alisema kuwa tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya hafla hiyo. Alisema kuwa hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa Msanii huyo kama balozi mpya wa MAÜA association.
"Mimi tayari nimeshafika huku na nina matarajio makubwa katika tamasha hili ambalo ni mara ya kwanza kwangu kushiriki katika nchi hii"Alisema
Alisema kuwa hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Wana-diaspora, viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Maüa association (MAÜA) ni taasisi iliyoundwa na Watanzania waishio ughaibuni (Ufaransa). MAÜA association ilianzishwa na kusajiliwa kwa sheria za mashirika ya kujitolea nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao. 

No comments

anonymous