Afande Sele adadavua post yake na kumjibu Mrisho Mpoto (Sauti)


Baada ya Mahakama Kuu ya Dar es Salaam kumkuta na hatia muigizaji Elizabeth Michael Maarufu kwa Jina la "Lulu" kuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba mwaka 2012 na kumuhukumu miaka 2 Jela, Mastaa wengi walimpost Lulu kumpa pole na kumtia moya juu ya tukio hilo, Lakini Afande sele Alikuwa tofauti kwa kuandika ujumbe mrefu na kumuangushia lawama marehem Steven Kanumba, Afande aliandika.. 

Nakumbuka vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya ndege anaejiandaa kuruka,Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West uliokua maarufu sana nyakati zile...Lkn wakati nikiwa back stage kabla sijapanda jukwaani huku usiku ukiwa umetamalaki yaani ule usiku wa manani au usiku wa manane kama wengi tulivyozoea kusema ingawa tunakosea nikashangaa nashikwa begani na mtu aliyekua nyuma yangu ambapo kulikua na watu wengi tu


...nilipogeuka niangalie ninani aliyenishika bega''Hammad"nikamuona Lulu michael aliyekua bado ni bint mdogo sana ingawa tayari alikua na umaarufu si haba labda kwa sababu ya hayo maigizo yao ambayo baadae wakayaita filamu au bongo movie...nilipomuona akaniamkia kwa bashasha namimi nikaitikia huku sura yangu nikiikunja na kuwa ya kuogofya kisha nikaamuuliza kwa ukali kidogo ni kwanini yupo pale ukumbini ktk muda ule ambao kwa umri wake hakupaswa kuwepo?..lulu hakua na majibu ya maana na papo hapo nikamtoa nje ya ukumbi na kisha nikamtuma dereva wangu wkt ule alikua home boy wangu ephraim nguzo aka bad card amrudishe nyumbani kwao haraka na ahakikishe mama yake amempokea...Bad alifanya hivyo kiroho safi akarejea ukumbini na akanimbia kuwa alitimiza yote niliyomuagiza ukizingatia na yeye badi tayari alikua na familia hivyo aliujua vyema uchungu wa mwana...lkn miezi michache baadae nikaja kupigwa butwaa baada ya kusikia kuwa et kale kabint lulu kumbe tayari kalikua na ukaribu usio wa kawaida na baadhi ya hao wasanii mabazazi wa maigizo wasiokua na utu wala aibu...niliumia sana moyoni nikiwa kama mzazi wa mtoto wa kike ninaempenda sana na kutamani kumuona akitimiza ndoto zake muhimu kwenye maisha kama kupata elimu kwa wkt muafaka...lkn niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar tena palepale ...mimi nilikua dar tena palepale sinza msiba ulipokuwepo...sikutaka kuvaa joho la unafki kama ilivyo kwa waTz wengi...kwangu hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake...leo kanumba amepumzika au anapambana na Mola wake kwa kutofuata yale maandiko yasemayo kuwa'TAMAA Ikichukua Mimba Huzaa Dhambi na Dhambi Ikishakukomaa Huzaa MAUTI...Kanumba amevuna alichopanda lkn Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso ktk maisha yake...MUNGU ni mwema atamuafu Lulu amalize kifungo chake salama kama alivyompa kanumba haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema...Mwisho wa siku wote wawili wabarikiwe kwa kutufundisha tuliobakia ili tuchague njia sahihi za kupita....DUNIA..GUNIA...No comments

anonymous