AIRTEL, UCSAF ZA WAELEKEZA NGUVU VIJIJINI

 

John Mukondya kutoka  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) akiongea na wakazi wa kijiji cha Matuli wakati kampuni ya simu ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na UCSAF walipotembelea kijiji cha kijiji cha Matuli kwenye wilaya Morogoro Vijijini kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano. Kijiji cha Matuli ambacho kina wakazi Zaidi ya 3,100 kimekuwa changamoto ya huduma ya mawasilaiano tangu kuanzishwa kwake.


Mbunge wa jimbo la Morogoro Vijijini Hamisi Taletale akionyesha jinsi wakazi wa kijiji cha Matelu wanapotumia mtu maalum kwa ajili ya kupata mawasiliano ya simu za mkononi wakati kampuni ya simu ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na UCSAF walipotembelea kijiji cha kijiji cha Matuli kwenye wilaya Morogoro Vijijini kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano. Kijiji cha Matuli ambacho kina wakazi Zaidi ya 3,100 kimekuwa changamoto ya huduma ya mawasilaiano tangu kuanzishwa kwake.


Mbunge wa jimbo la Morogoro Vijijini Hamisi Taletale akifyeka kwenye eneo ambalo litajengwa mnara wa mawasiliano kwenye kijiji cha Matuli  wakati kampuni ya simu ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na UCSAF walipotembelea kijiji cha Matuli kwenye wilaya Morogoro Vijijini kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano. Kijiji cha Matuli ambacho kina wakazi Zaidi ya 3,100 kimekuwa changamoto ya huduma ya mawasilaiano tangu kuanzishwa kwake.


Mbunge wa jimbo la Morogoro Vijijini Hamisi Taletale akionyesha jinsi wakazi wa kijiji cha Matelu wanapotumia mtu maalum kwa ajili ya kupata mawasiliano ya simu za mkononi wakati kampuni ya simu ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na UCSAF walipotembelea kijiji cha kijiji cha Matuli kwenye wilaya Morogoro Vijijini kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano. Kijiji cha Matuli ambacho kina wakazi Zaidi ya 3,100 kimekuwa changamoto ya huduma ya mawasilaiano tangu kuanzishwa kwake.


Alhamisi Morogoro 27 Mei 2021 …. Wananchi wa kijiji cha Matuli kwenye wilaya Morogoro Vijijini, jimbo la Morogoro kusini mashariki wameipongeza kampuni ya simu ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa jitahada zao za kuhahakisha wanafikisha huduma ya mawasiliano kwenye kijijini chao ambacho kimekuwa changamoto ya huduma ya mawasilaiano tangu kuanzishwa kwake.

 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo hilo Hamisi Taletale wakati kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote –UCSAF walipotembelea kijiji hicho kwa lengo ya kuanzisha ujenzi wa mnara wa mawasiliano ambayo utafanya kijiji hicho cha Matuli chenye wakazi Zaidi ya 3,100 pamoja na vijiji vya jirani vyenye wakazi zaidi ya 5,500 kupata mawasiliano ya uhakika.

 

Kwa sasa hali ilivyo ni kwamba wananchi wakitaka kufanya mawasiliano ulazimika kwenda eneo moja lenye mti maalum uliofungwa na makopo kwa ajili ya kupata mtandao wa mawasiliano. “Kwa kufanya hivyo, wananchi wanakosa ile faragha ya mawasiliano na wengine pia hutumia muda mwingi kwa kusafiri kwenda eneo hilo’, alisema Taletale.

 

Aliongeza, “Tunajua kujenga miundo mbinu kama hii ni gharama sana lakini naomba niwaahidi ya kwamba sisi wananchi tutakuwa walinzi kuanzia kwenye ujenzi mpaka pale mnara utakapokamilika kwani kukamilika kwake kuna manufaa kwetu sisi wananchi wa Matuli’.

 

Tunayo furaha kubwa na tunatoa pongezi kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Matuli kwa kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote –UCSAF kwa kuja na kuanza ujenzi wa mnara ambao ukikamilika utakuwa umetatua changamoto ya mawasiliano kwenye kijiji chetu cha Matuli pamoja na vijiji vya jirani zaidi ya kumi kama vile Kwaba, Dibuzi, Lilongwa, Lubumo, Magela, Selegeti A, Selegeti B hadi Visaraka .

 

Kwa upande wake, John Mukondya kutoka  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) alisema “Serikali ya awamu imekuwa ikitumia juhudi kubwa kuhakikisha kuwa maeneo ya vijijini yamefikiwa na huduma za mawasiliano. Ninayo furaha kubwa siku ya leo kuwapongeza Airtel Tanzania kwani wamekuwa wakiunga juhudi zetu na leo hii tunajenga mnara utakaokuwa ni  msaada mkubwa kwa eneo lote la Matuli pamoja na vijiji vya jirani’

 

Mukondya aliongeza kuwa “Wananchi wanapokuwa na uhakika wa mawasiliano inawawezesha kufanya shunguli zao za kila kwa unafuu. Vile vile inaweza kuwainua kiuchumi kwani kwa maeneo haya wananchi wengi ni wakulima, kwa hivyo inakuwa ni rahisi kuweza kupata masoko ya mazao kwa kupitia simu zao za mkononi kuliko hapo awali ambapo walikuwa wanapeleka mazao yao sokoni bila kujua bei yao”.

 

 Akizungumza kwenye kijiji hicho cha Matuli baada ya kutangaza kuanza kwa ujenzi wa mnara huo, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando alisema mnara wa mawasiliano ambao ujenzi wake umeanza mara moja ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kushirikiana na UCSAF kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wananchi, hususani maeneo ya vijijini au pembezoni mwa mji

  

“Dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuhakikisha tunapanua wigo kwa kuzindua minara ya mawasiliano na kuwezesha maeneo mengi nchini kufikiwa na kupata huduma bora za mawasiliano, alisema Mmbando.

   

“Tunafanya hivi tukiamini kuwa shughuli za kilimo na uvuvi pamoja na kibiashara ndizo nguzo kuu ya kukua kwa uchumi wa wananchi  wa maeneo haya, hivyo hatua ya kuwaunganisha kupitia mawasiliano haya ni sehemu muhimu ya kuwawezesha kutimiza matakwa yao ya kiuchumi’’ alimaliza kusema Mmbando.

No comments

anonymous