Picha: Mwili wa Ndikumana ulivyopumzishwa katika nyumba ya milele.

Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi  Ndikumana Katauti, umezikwa jana katika makaburi yaliyopo kwenye mji wa Nyamirambo nchini Rwanda.
Ndikumana ambaye pia ni baba wa  watoto waili huku mmoja akiwa amezaa na Irene Uwoya, amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon Sport, ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.
Taarifa zaidi zinasema kwamba Irene Uwoya hakuwahi kuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Ndikumana alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake nchini Rwanda, na kuacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa soka na watu wake wa karibu, kutokana na kifo chake kilichotokea ghafla bila kuumwa.
Angalia picha.

Mama yake marehemu Ndikumana akilia kwa uchungu.Baba yake Ndikumana


No comments

anonymous