DJ Supreme la Rock kutua Dar kwa ajili za ziara kubwa ya mziki ya siku tatu


Mburudishaji wa Kimarekani, kutokea Seattle, Washington Dj Supreme anatarajiwa kuitingisha Dar wiki hii. Ziara hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa DJ Vasley, DJ Sma na DJ FU itafanyika kwa siku tatu katika maeneo mbalimbali na hoteli jijini Dar-es-salaam.
Dj Supreme ambaye kwa sasa amekusanya kazi zaidi ya 50,000 anatarajiwa kuongeza nyingine akiwa hapa Tanzania.

"Niliacha kuhesabu kazi nilizozikusanya zilipofika 50,000 lakini bado kuna kazi nyingi zinazozitaka ambazo sijazipata. Kimsingi lengo langu kubwa nikiwa katika ardhi mama ya Afrika ni kukusanya kazi zenye asili ya Afrika za Vinyl” Alisema Dj Supreme.
Anaongeza kwa kusema "Ninatafuta funk, soul, disco, boogie, high life, kazi za makundi maarufu kama Asiko, Geraldo Pino, Kelenkye, Marijata, Rob, Witch, na William Onyebor.Huenda zipo mahali fulani kwenye nyumba ya mtu zikiwa zimajaa vumbi. Kama mtu anaweza kunisaidia kuzipata kazi izo nitashukuru sana”

Matukio haya ya mziki yanaandaliwa na kampuni mpya ya uandaaji wa Matukio mbalimbali jijini Dar-es-salaam ijulikanayo kama Xfinity Entertainment. Matukio rasmi ya Dj Supreme yatafanyika tarehe 30 Novemba (Alhamisi), Desemba 1 (Ijumaa) na Desemba 2 (Jumamosi). Matukio hayo yamefadhiliwa na na Jameson na Red Bull kwa ushirikiano na Clouds Media Group kama mshirika rasmi kwa upande wa vyombo vya habari.

Xfinity ni muunganiko wa jazz, funk, soul na lingala zikipambwa na bongo flava. Kampuni hii ya usimamizi wa matukio na watu imeanzishwa mwaka huu wa 2017 ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya burudani kwa watanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kwa sasa Xfinity inafanya matukio matatu kila wiki katika eneo la kifahari la Masaki, Dar-es-salaam na katikati eneo la kibiashara la mji. Kampuni hii inaongozwa na DJ Vasley, DJ Sma na DJ FU.
Ma DJ hao wa Xfinity wamefanya kazi na wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania kama Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Juxs MiCasa, Black Motion, Tinie Tempah, Future pamoja na kufanya kazi na Ma DJ mbalimbali wa kimataifa.

Ratiba ya Dj Supreme nchini itahusisha pia kutembelea maeneo ya kihistoria ya Zanzibar. Dj huyo mzaliwa wa Los-Angeles pia atatembelea Clouds Media Group kama sehemu ya ziara yake ya vyombo vya habari.

Dj Supeme anayejulikana zaidi kama Supreme la Rock atapata fursa ya kukutana na mastaa wa ndani akiwemo Dj-Ommy ambapo atajifunza utamaduni wa kiswahili.
Atapata nafasi ya kulinganisha mbinu zake na Dj D-Ommy pale watakapokutana. Ratiba imeshaandaliwa kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wataweza kupata taarifa juu ya ziara yake hiyo na maonyesho mbalimbali atakayoyafanya kuonyesha uwezo wake.

"Ninafuraha kuja Afrika Mashariki na Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mengi kuhusu eneo hili. Natumai nitapata fursa ya kujifunza utamaduni wa kiswahili na mziki, kukusanya kazi za kibongo na kubadilishana uzoefu na Ma DJs wa Tanzania.” Alihitimisha Dj Supreme


No comments

anonymous